.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZILIZO CHEZWA LEO LIGI KUU ENGLAND

OZIL
Ligi kuu ya England imeendelea hii leo kwa michezo iliyopigwa kwenye viwanja nane ambapo timu 16 zilikuwa uwanjani .
Katika mchezo wa kwanza mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester United waliwafunga vijana waliopanda daraja Crystal Palace mabao mawili bila .
Robin Van Persie akifunga mkwaju wa penati kuipa United bao la kwanza kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Robin Van Persie akifunga mkwaju wa penati kuipa United bao la kwanza kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Mabao ya United kwenye mchezo huo yalifungwa na Washambuliaji Robin Van Persie na Wayne Rooney.Robin Van Persie alifunga bao lake baada ya mwamuzi kuizawadia United Penati kufuatia kiungo Ashley Young kuangushwa na kiungo wa kimataifa wa Afrika Kusini Kagisho Digkacoi ambaye alionyeshwa kadi nyekundu huku Wayne Rooney akifunga kwa mpira wa adhabu ndogo toka umbali wa mita 30.
Wayne Rooney akifunga bao la Free Kick .
Wayne Rooney akifunga bao la Free Kick .
Kwingineko Arsenal waliwafunga Sunderland  3-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Sunderland The Stadium Of Light . Arsenal walianza kufunga bao lao kwneye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud ambaye hii leo amefunga bao lake la nne kwenye ligi kuu msimu huu akipata pasi toka kwa Mesut Ozil ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza . Sunderland walisawazisha bao hilo kupitia kwa kiungo Craig Gadner kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Arsenal Laureant Koscielny kumchezea rafu mchezaji wa Sunderland . Arsenal walirejea mchezoni na kuongeza mabao mawili ya haraka yaliyofungwa na kiungo Aaron Ramsey.
Aaron Ramesy alifunga mabao mawili kwenye mechi ya Arsenal na Sunderland .
Aaron Ramesy alifunga mabao mawili kwenye mechi ya Arsenal na Sunderland .
Newcastle United waliwafunga Aston Villa 2-1 huku wafungaji wakiwa Hatem Ben Arfa na Yoan Goufran kwa Newcastle na Christian Benteke akifunga bao pekee la Villa.
Tottenham Hotspurs waliwafunga Norwich City 2-0 . Mabao ya Spurs yalifungwa na Gylfi Siggurdson ambaye alifunga mabao yote mawili.
Mechi ya Hull City na Cardiff City timu mbili ambazo zimepanda daraja msimu huu iliisha kwa sare ya 1-1 . Hull walianza kufunga kupitia kwa Curtis Davies kabla ya Peter Wittingham hajaisawazishia Cardiff City kwenye kipindi cha pili .
Fulham na West Bromwich Albion nao walitoka sare ya 1-1 . Wafungaji kwenye mchezo huo walikuwa Steve Sidwell kwa Fulham na Gareth McAuley kwa West Brom.
Mchezo kati ya Manchester City na Stoke City uliopigwa huko Brittania Stadium uliisha kwa sare ya bila kufungana
Stoke City na Man City walitoka sare ya 0-0.
Stoke City na Man City walitoka sare ya 0-0.

Matokeo ya Mechi Za Ligi Kuu Ya England.
Manchester United 2-0 Crystal Palace .
Aston Villa   1-2   Newcastle United .
Tottenham   2-0  Norwich City .
Sunderland  1-3   Arsenal.
Hull City       1-1   Cardiff City .
Fulham         1-1   West Bromwich Albion.
Stoke City    0-0   Manchester City.
 Chelsea       0-1   Everton


SOURCE: MILLARD AYO

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad