.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Majambazi wavamia Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani

Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani, Dar, leo imevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kupora kiasi kikubwa cha pesa. 
(Picha haiusiani na Stori)
"Wamekuja na Noah nyeusi wakapark kama wateja. Walikua wawili, mmoja akapanga msitari mwingine akaenda kujaza fomu za kuchukulia hela. Yule alopanga msitari akafunga mlango na yule Askari akakunjwa akanyang'anywa alarm. Yule alokuwa anajaza fomu kawambia wateja nyote lala chini, alikua anamjua mwenye ufunguo, wakasema Anna leta huo ufunguo. Akataka kugoma walipomnyoshea mtutu akatoa. wakaingia Kwenye chumba cha hela wakakomba hela zote wakapakia kwenye Noah."(inadaiwa ni zaidi ya milioni 900) 

Wakawaaga na kusema iteni hao Polisi wenu. Hamna aliyeumizwa zaidi ya Askari kukunjwa kunjwa alipotaka kubonyeza alarm.


Source:JamiiForum
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad