Saturday, 10 August 2013

AMPIGA MKE WAKE RISASI KISHA KUJIPELEKA POLISI

Mbulula anaetambulika kwa jina la Derek Medina  kutoka Florida amemuua mke wake siku ya alhamisi na kuandika kuhusu tukio hilo katika ukurasa wake wa facebook
derek madina akiwa na mpenzi wake aliye muua jeniffer alfonso
Mara baada ya kuandika jamaa huyo alijipeleka katika kituo cha polisi na kuwaambia askari walio kua katika kituo hiko kua amefanya mauaji ndipo hapo askari walipo enda katika eneo la tukio na kumkuta mwanamkee huyo aliepigwa risasi mbili amanguka jikoni akiwa tayari ameshakata roho


Jamaa huyo amesema chanzo cha yeye kumuua mke wake ni kutoka na kuchoshwa na mangumi alio kua akipigwa na mke wake huyo
Mwanamke huyo alikua na miaka 26 na mapolisi walikuta mtoto wa miaka 10 ndani ya eneoo ya tukio lakini alikua hana jeraha hata moja...

Medina amesema kwamba walikua na ugomvi ndipo alipo amua kupanda juu na kuchukua bastora yake na kumtishia kisha akarudi juu chumbani ndipo hapo mwanamke huyo alipo mfata na kuanzz kumpiga ngumi kisha Jeniffer akaondoka na kurudi jikoni ndipo hapo Derek Medina alipo amua kumfata bila ya bastora na kumkuta Jeniffer ameshika kisu ..Derek akajaribu kumpokonya na kufanikiwa lakini Jeniffer akaanza kumpiga ngumi Derek ...Hapo sasa uvumilivu ukamshinda kijana huyo na kuamua kwenda chumbani kuchukua bastora na kurudi kufanya akili yake ilicho mwambia kufanya.... - See more at: http://williammalecela.blogspot.com/#sthash.XRcqBHOt.dpuf

No comments:

Post a Comment