Wapangaji wa nyumba moja iliyopo Kijitonyama mkabala na Kituo cha Polisi cha Mabatini jijini Dar es Salaam, leo wametupiwa vitu nje na mnunuzi mpya wa nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi. Imedaiwa kuwa nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mtu mmoja aliyetajiwa kwa jina la Juma Telela, ambaye alimuuzia mtu mwingine bila kuwashirikisha wapangaji. Katika sakata hilo wapangaji hao wamedai kuibiwa vitu vyao na kundi la vijana waliopewa kazi ya kuibomoa nyuma hiyo.
No comments:
Post a Comment