.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

FEZA KESSY AKIWA BOTSWANA


Baadhi ya watu hawakutarajia sana kama mapenzi ya Feza Kessy na Oneal wa Botswana yangepamba moto kiasi hiki, mpaka Feza kumfata mpenzi wake nchini kwao Botswana fasta tu baada ya kutua Tanzania.

Wakati anatolewa BBA, Feza alikiri kumpenda kweli Oneal na alionyesha kabisa anahitaji Oneal awe mwanaume wake wa maisha.


Oneal, Feza and friends


Taarifa ikufikie kwamba Feza ambae ni mama wa mtoto mmoja, ameshafika Botswana na kupokelewa kwa shwangwe na Mawifi na Mashemeji waliojitokeza kuanzia uwanja wa ndege.



Kama hiyo haitoshi, Feza ameonekana kuwa na furaha kupitiliza... ametumia page yake ya twitter kueleza sehemu ya hisia zake juu ya mapokezi na mpenzi wake Oneal.

Mapokezi mazuri hayajaonekana Airport tu au barabarani bali mpaka kwenye mtandao wa twitter ambako Wabotswana wengi wamefurahishwa na muunganiko wa wawili hao ambao mapenzi yao yameanzia kwenye shindano la BBA 2013 walikokutana kwa mara ya kwanza.


Motamma, Feza and Oneal


Oneal na Feza watajumuika na mashabiki wao kwenye chakula jioni kwenye Oneza Gala Dinner 22 August, ambapo kila shabiki atakaeingia atalipia kiingilio.



Je Feza ndio amekwenda Botswana moja kwa moja? Itakua kama Elizabeth Gupta ambae kaolewa na Kevin wa Nigeria? 
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad