Monday, 12 August 2013

MSANII ROSE NDAUKA APIMA UKIMWI NA HAYA NDIO MAJIBU YAKE.



Mwanadada Rose Ndauka ambaye hivi karibuni aliingia katika skendo ya kimapenzi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayechipukia, ameamua kuwa mmoja wa wasanii wachache wa Sanaa ya Filamu nchini kuamua kuanika wazi majibu ya vipimo 
vyake vya gonjwa hatari la ukimwi nchini.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmmoja wa kijamii, Rose aliweka majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa wiki kadhaa zilizopita katika hospitali ya TMJ iliyopo jijini Dar es salaam, vikionesha kuwa mwanadada huyo yu SALAMA kabisa na safi kiafya ama HIV NEGATIVE kwa mujibu wa vipimo hivyo.
Katika picha hiyo Rose ndauka aliandika anamshukuru Mungu sana kwa majibu hayo.


No comments:

Post a Comment