Mchungaji Albogast baada ya kuachiwa huru.
Wachungaji watano wa makanisa ya Pentekoste waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi Tanzania na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao aitwaye Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia wakati wengine wanne wakihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.
Kesi hiyo ambayo imeunguruma kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar takribani miaka minne, kupitia kwa hakimu wake, Aloyce Katemana ilitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi na Jamhuri. Vilevile kwa wale wote waliopanda katika taasisi hiyo wote wameonekana kutenda kosa, hivyo hawana chao.
No comments:
Post a Comment