.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

HAWA NDIO WANAMUZIKI WA BONGO WALIOINGIZA KIPATO CHA HALI YA JUU

Biashara ya muziki Tanzania imeendelea kupanuka kwa kiasi
kikubwa, na wasanii wenye hits, majina, connection, bahati na
sababu zingine wameendelea kuingiza fedha nyingi kutokana na
muziki wao.
Njia kubwa na za uhakika zinazowapatia mapato wasanii ni
pamoja na malipo ya show, malipo ya ringtones, endorsements
(mfano kuwa mabalozi wa brands mbalimbali na kufanya
matangazo) na wengine kupata kipato kupitia biashara
walizozianzisha.
Kama njia kubwa zingine mbili za kuwaingizia kipata wasanii
wengi duniani zingefanikiwa nchini, wasanii wetu wangekuwa
mbali zaidi. Njia hizo ni mauzo ya albam za muziki na malipo ya
mirahaba kutokana na matumizi ya nyimbo zao kwenye kumbi za
starehe na kwenye vituo vya radio au TV.
Licha ya kuwepo kasoro hizo, bado Bongo Flava imebadilisha
maisha ya wasanii wengi.
Bongo5 imejitahidi kukusanya kadri iwezavyo, data za uhakika
kutoka kwa watu walio karibu na wasanii kadhaa wa Tanzania
kutaka kufahamu, kiasi walichoingiza, malipo waliyoyapata
mwaka huu na data zingine zingine, kuandaa orodha hii ya wasanii
5 walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.
Wafuatao ni 5 waliongiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.
1. Diamond Platnumz
Hakuna ubishi kuwa, mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii
aliyeingiza fedha nyingi zaidi. Pesa nyingi ya Diamond imetokana
na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi. Kwa uhakika,
mwaka huu pekee, Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi
bilioni 1.
Kwa show za ndani peke yake, Diamond hutoza si chini ya shilingi
milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2. Hivyo
tangu mwaka uanze, Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni
40 kila wiki. Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile
za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu, show ya
Burundi na Congo, show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa),
show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na
show ya Malaysia wiki iliyopita.
Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno
zisizo na idadi, ukiachana na zile za kawaida, Diamond aliingiza
shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila
show alilipwa shilingi milioni 10. Ndiye msanii aliyelipwa fedha
nyingi zaidi kwenye ziara hiyo.
Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013, show za promotion za
Tigo na makampuni mengine, Tamasha la Matumaini, show ya
Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club, show yake na Nay wa
Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu,
Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake
kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi
kufurika.
Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’
ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi
wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo
zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show, Diamond amekuwa
akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo
kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi
milioni 20. Kwa mujibu wa Push Mobile, akaunti ya Diamond kwenye
kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine
yeyote wa Bongo Flava.
Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza
wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi
kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya
shilingi.
Ikumbukwe pia, Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo
ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi, lakini ni fedha
inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo
Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio
Africa.
2. Lady Jaydee
Huwezi amini, vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu
kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi
mno. Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya
mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi
milioni 100. Haikuishia hapo, albam yake Nothing But The Truth
ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa
Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake
hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki
mwenye show nyingi zaidi pia. Lady Jaydee ametumbuiza kwenye
karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi
milioni 25.
Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo
ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye
Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid
Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika
Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za
albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa
kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka huu pia, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya
kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini,
iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya
mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge,
imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi
wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa
bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show
yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake
ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika
waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni
ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.
Coke Studio Africa – the new, exciting music show featuring
incredible live performances by the very best in Africa
3. AY
Humsikii sana rapper huyu kwenye show za Tanzania. Tofauti na
wasanii wengine, fedha anazoingiza AY zinatokana zaidi na
endorsements na biashara zake anazofanya. Pesa nyingi
alizoingiza zimetokana na mkataba wa mwaka mmoja na Airtel wa
ubalozi uliokamilika mwezi May mwaka huu.
Katika ubalozi huo wa Airtel Africa, AY aliungana na wasanii
wengine watatu wa Afrika ambao ni pamoja na Papa Wemba,
Tuface na Daddy Owen wa Kenya. Katika mkataba huo AY alilipwa
dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 129.
Rapper huyo wa ‘Machoni Kama Watu’ ni balozi pia wa bia ya
Peroni ya Italia na kupitia mkataba huo, AY ameingiza mkwanja
mwingi. AY pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha Mkasi
kinachoendeshwa na Salama Jabir. Kipindi hicho kina wadhamini
wawili, Cocacola na Airtel na hivyo kupitia mgawanyo wa mapato,
AY amekuwa akiingiza pia fedha ya kutosha.
AY ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na
kuandaa show, matangazo, kuleta wasanii wa nje na mambo
mengine. Mwaka huu pekee, ikishirikiana na kampuni ya SK
Entertainment, kampuni yake imeandaa show kibao zikiwemo zile
zilizofanyika Elements Lounge ambapo Avril, Prezzo, Huddah
Monroe na J-Martins wamewahi kuhudhuria.
Maisha ya kawaida ya rapper huyu ndio yanayowafanya watu
wengi wasijue ukubwa wa kile anachokiingiza. Macho yake
ameyaelekeza zaidi kwenye uwekezaji na anawekeza haswaa.
Kuna tetesi kuwa, AY anajenga ghorofa lake maeneo ya
Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anasemekana kuwekeza pia
mkoani Mtwara alikonunua ardhi ya kutosha. Mungu ndio anajua
ni wapi alikowekeza tena.
4. Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini
Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya.
Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000
ambazo ni sawa shilingi milioni 81.
Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo, tayari Ommy
ameshaingiza shilingi milioni 50. Kwenye show yake ya hivi
karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas, Ommy
alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama
zote. Watu 1,770 walihudhuria show hiyo.
Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita
ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya
shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi, amekuwa na uhakika wa
kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili
Music Tour.
Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5, Ommy
alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa
endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya
uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal
kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye
thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja
vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Hivi
karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.
5. Madee
Hii inaweza kuwa surprise kwa wengi lakini Madee ni mfano tosha
wa jinsi single moja inavyoweza kubadilisha maisha ya msanii.
Tangu atoe single yake, Sio Mimi, Madee ameshaingiza si chini ya
shilingi milioni 200.
Mwaka huu ameshafanya show 10 za kampeni ya Tigo ambapo kila
moja alilipwa shilingi milioni 3, show 15 za Airtel kwa kiwango
hicho hicho. Alifanya show mbili za kampeni za Coca Cola, ile ya
uzinduzi wa Coke Zero na Cocacola Bonanza Mlimani City. Bado
ameendelea kufanya show za Fiesta 2013. Madee pia alikuwa
miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Fuse ODG
iliyofanyika September 7 kwenye viwanya vya ustawi wa jamii
jijini Dar es Salaam.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad