Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.
Mwanamke huyo amekamatwa akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa
kwa ndege ya Ethiopian Airways na aliingia hapa nchini
Agosti 30 akitokea Nigeria.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya
Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi
kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye ofisi ya mkemia
Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo na thamani yake...
swali ni ..JE ALIKUA ANAPELEKA KWA NANI ??
0 comments :
Post a Comment