.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

IDADI YA MABILLIONEA AFRIKA NI 55

 angola a4472
Afrika ina mabilionea 55 idadi hii ikiwa kubwa zaidi ya ile iliyosemekana siku za nyuma. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya jarida la Ventures financial nchini Nigeria.
Kati ya hawa mabilionea watatu ni wanawake , mamake Rais wa Kenya , mwanawe rais wa Angola na mfanyabiashara wa mafuta pamoja na mitindo ya (HM)
mavazi nchini Nigeria.

Mwanamume tajiri zaidi ni Aliko Dangote,wa Nigeria mwenye mali ya thamani ya dola bilioni 20 katika biashara zake.
Hii bila shaka itazua mjadala kuhusu pengo lililopo kati ya matajiri na maskini barani Afrika.
Mnamo mwezi Aprili, benki ya dunia ilisema kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini mkubwa barani Afrika imeongezeka katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kutoka watu milioni 205 hadi watu milioni 414 .
Ripoti iliyotolewa awali, na shirika la utafiti la Afrobarometer ilipendekeza kuwa ukuwaji wa kiuchumi barani Afrika unawanufaisha wachache sana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Tomi Oladipo, hii ni mara ya kwanza jarida lenye ushawishi la Ventures Nigeria kuchapisha orodha ya waafrika wenye utajiri mkubwa,
Mabilionea hao 55 waliotajwa na jarida hilo ni wengi zaidi kuliko idadi iliyochapishwa na jarida la maswala ya kifedha la Marekani mwaka jana.
Watafiti wa jarida hilo walitumia mbinu tofauti na jarida zengine kufanya utafiti wao na ndio maana wakaja kugundua idadi hiyo kubwa ya matajiri wa kiafrika.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad