Anafahamika kama Snura Mushi ni wanadada mwenye vipaji vingi ndani
ya tasnia ya bongo movies. Pamoja na kuwa mwigizaji aliyekuja kwa kasi
sana pia Snura ni mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya vizuri sana
sokoni kwa nyimbo zake mbalimbali zenye mahadhi ya pwani mithili ya
mduara. Pamoja na kuwa na umbo na sura nzuri ya kuvutia snura pia
amekuwa akitawala sana vichwa vingi vya habari,magazeti na redio
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukata kiuno kwenye nyimbo zake.
Snura Mushi (Jina lake halisi) alizaliwa tarehe kumi na mbili (12)
mwezi wa kwanza (1) mwaka 1984 Jijini Dar es salaam ambako aliweza kukua
na kupata elimu yake hapo hapo Dar es salaam.
Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya ITUNYAMA, na pia kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa chini ya director Tuesday Kihangala “Mr Chuzi”. Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa huwa anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari zinazomuhusu ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli. Katika maisha yake ya kila siku Snura hupendelea sana kukaa ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.
0 comments :
Post a Comment