.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MTOTO WA WAZIRI LUKUVI AJERUHIWA KWA TUHUMA ZA UJANGILI

MTOTO wa kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi, aitwaye Tomm Malenga, ambaye ni katibu wake, amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuhusishwa na ujangili.
Habari zilizopatikana mjini hapa, juzi Jumapili, Oktoba 27, mwaka huu, zinasema akiwa ofisini kwake siku hiyo, Tomm alifuatwa na maofisa wa Wanyama Pori kwa kile kilichotajwa kuwa anahusika na ujangili.
“Walifika na kumkamata kisha wakaanza kumpiga, tena palepale ofisini kwa Lukuvi. Amevunjika vidole vya mguu na mkono wake mmoja hauko sawa baada ya kipigo hicho,” alisema mtoa habari wetu.
Tomm hakupatikana ili kuzungumzia sakata hilo lakini waziri Lukuvi alifafanua baada ya kuzungumza na mwandishi wetu ambapo alisema kilichofanyika anakijua na kwamba ni njama za wabaya wake.
“Sikiliza bwana, licha ya Tomm kuwa msaidizi wangu wa jimboni ni mtoto wa marehemu kaka yangu. Wanasema eti ametajwa kwenye ujangili; sasa kutajwa tu, unawezaje kwenda kumchukua mtu ofisini kwake, tena kwa kumpiga? Huo siyo utawala wa kisheria,” alisema waziri Lukuvi.
Alisema, mtu aliyemtaja Tomm ni Gedi ambaye alikuwa wa kwanza kukamatwa kwa ujangili na akasema amekuwa akishirikiana na mwanaye.
“Ukweli ni kwamba huyo Gedi ana usongo na mimi, kwani huwa ananipinga tangu mwaka 1995. Aliwahi kugombea udiwani, tukagundua kuwa ni Msomali, tukamfuta. Nadhani anatumia mwaya huo kunichafu mimi na familia yangu,” alisema Lukuvi.
GPL
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad