Ghana imefuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-3, baada ya kufanya kazi nzuri katika mchezo wa kwanza mjini Kumasi mwezi uliopita na sasa watakwenda Brazil kujaribu kuendeleza mafanikio ya fainali zilizopita Afrika Kusini mwaka 2010 walipofika Robo Fainali.
Misri,
waliokuwa wakicheza nyumbani kwa mara ya kwanza mjini Cairo ndani ya
miaka miwili, walianza vizuri na kuongoza kwa 2-0, mabao ya mshambuliaji
wa Wigan Athletic, Amr Zaki na Gedo.
Lakini Kevin-Prince Boateng akaifungia Ghana bao la kufutia machozi dakika za lala salama na kufanya matokeo yawe 7-3, baada ya awali kushinda 6-1 nyumbani.
Ghana imeungana na timu nyingine tatu za Afrika kufuzu kwenye fainali hizo, Ivory Coast, Nigeria na Cameroon na mchezo kati ya wenyeji Algeria na wageni Burkina Fasso unaoendelea hivi sasa utakamilisha idadi ya timu tano zitakazoliwakilisha bara hili kwenye fainali hizo.
Katika mchezo wa kwanza, Burkina Faso ilishinda 3-2 nyumbani, maana yake Algeria hata wakishinda 1-0 leo nyumbani kwao, watafuzu pia.

No comments:
Post a Comment