HII NDIO HABARI KUHUSU GARI JIPYA KABISA LINALOJIENDESHA LENYEWE:
Taarifa
ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kwenye headlines
ni kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa
jaribio la gari
walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa
limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya
aina mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za
barabarani, taa za kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka
barabara.
Nissan
wamesema wanalengo la kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa,
hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors
zinazofanikisha kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio
maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga
mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking
ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta
parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako
unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.
Baada
ya kutazama hizo picha hapo juu, unaweza kutazama hii video
kujiridhisha kikamilifu aisee japo hii video sio ya majaribio
yaliyofanyika saa kadhaa zilizopita..
No comments:
Post a Comment