.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Abdul Ngarawa, Mkurugenzi Mstaafu RTD awafunda watangazaji, wanahabari


Picture
 MKURUGENZI Mstaafu wa iliyokuwa Radio Tanzania RTD Bw. Abdul Ngarawa amesema kuwa weledi wa kazi za uandishi wa habari umeporomoka kutokana na baadhi ya waandishi wa habari kutotumia vipaji vyao na badala yake kuiga sauti za watangazaji wengine kwa kukosea. 

Bw. Ngarawa amesema kuwa kazi ya uandishi na utangazaji mbali ya kuwa ni taaluma bali pia inahitaji kipaji cha mtu binafsi na kwamba waandishi wanaopenda kuiga sauti za watangazaji wa zamani wanakosea: ‘’Unapaswa kutangaza wewe kama wewe ili watu wakukubali wewe kama wewe uwe na utambulisho wako mwenyewe bila kuiga lahaja na sauti za wengine,’’anasema.

Alisema kuwa watangazaji wa sasa wanapaswa kujitahidi kutangaza kulingana kutokana na mazingira ya sasa kwa kujifunza zaidi na kufuatilia vyombo vingine vya habari kwa kufuatilia sera na maadili yao kwa nia ya kuboresha taaluma na weledi katika kazi ya Uandishi wa Habari na utangazaji. 
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad