CHUCHU AJICHORA TATUU YA RAY, RAY AJIBU
KATIKA hali inayoonesha kuna kitu kikubwa kinakuja mbeleni, msanii wa
filamu, Chuchu Hans amejichora ‘tatuu’ inayosomeka kwa jina la Ray huku
anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ naye akiwa amejichora
tatuu inayosomeka kwa jina la Chuchu.
Ray na Chuchu.
Picha ambazo gazeti hili limezinasa zinawaonesha wawili hao wakipigia
‘promo’ uhusiano wao huku wadau wengi wakiyafananisha mapenzi yao na ya
njiwa.
Ili kujua undani juu ya jambo hilo, mwandishi wetu aliwatafuta
wasanii hao ambapo Chuchu alionekana kukerwa na swali hilo na kujibu kwa
ufupi kuwa hataki kusumbuliwa.
“Hivi hamchoki kufuatilia maisha ya watu jamani? Naomba mniache,” alisema Chuchu Hans.
Kwa upande wa Ray, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment