.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

UZUSHI WA KIFO CHA MZEE SMALL, SHILOLE YAMKUTA!!! soma zaidi hapa



MSANII wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuandika juu ya uzushi wa kifo cha msanii mkongwe,  Said Ngamba ‘Mzee Small’ kupitia mtandao wa Instargram.
   
Said Ngamba ‘Mzee Small’ aliyezushiwa kifo
Shilole ambaye baada ya kugundua kuwa hakuwa sahihi kuandika juu ya kifo hicho kwani haikuwa kweli, alilazimika kukanusha na ndipo akaanza kuporomoshewa ‘mvua’ ya matusi.

Baadhi ya maneno makali yaliyoandikwa mtandaoni humo kumtukana  Shilole, ambayo hayawezi kuandikika kwa kuzingatia maadili, yalimtaka kujiepusha na tabia ya kudandia na kueneza mambo pasipo kuyafanyia uchunguzi.

Mwandishi wetu alipomtafuta msanii huyo kuzungumzia juu ya suala hilo, alikiri kuandika juu ya kifo hicho huku akionesha majuto ya hali ya juu.

Ni kweli niliandika maneno ya taarifa za kifo cha Mzee Small, japo nilikuwa nikiandika jinsi ambavyo msanii huyo amezushiwa kifo, sasa watu wakadhani mimi ndiye nimeandika kwa kujitungia, najuta sana kuchapisha ujumbe huo,” alisema Shilole.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad