.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

CHELSEA YAIPIGA BAO LA KISIGINO MAN U KWA DIEGO COSTA

soka 7ab46
KLABU za Chelsea na Atletico Madrid zimekubaliana kubadilishana wachezaji, Diego Costa ahamie Stamford Bridge msimu ujao, kwa mujibu wa vyombo habari Hispania.
Kipa wa Blues, Thibaut Courtois, anayecheza kwa mkopo Atletico, amekuwa akizungumziwa na wengi kama mlinda mlango hodari kinda Ulaya, baada ya kudaka vizuri akiwa na klabu hiyo ya Hispania kwa misimu mitatu.

Lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka 21 angependa kubaki Madrid, na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji nyota, Costa arejee. Kocha wa Manchester United, David Moyes alitumai kumpata mshambuliaji huyo Old Trafford.
Costa amefunga mabao 19 katika La Liga msimu huu, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real.
Kipaumbele cha Mourinho katika usajili huu ni mshambuliaji, na Mreno huyo amegoma kuondoka Januari.
Chelsea ilitaka kipa Courtois asaini Mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kuchezea timu ya Stamford Bridge, lakini Mbelgiji huyo angependa kuchezea klabu kwa Mkataba wa kudumu badala ya mkopo.
Courtois awali alisema atarejea Chelsea tu kuwa kipa namba moja mbele ya Petr Cech. Chanzo: binzubeiry

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad