.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

OPERASHENI TOKOMEZA: WACHINA WATEKETEZA MENO NA PEMBE ZA TEMBO


OPERESHENI TOKOMEZA
China yateketeza Tani 6 za meno ya Tembo kuunga Mkono juhudi za kupambana na tatizo la Kuangamizwa kwa Tembo Duniani. Inakuwa nchi ya tatu kufanya hivyo baada ya Marekani kuanza kufanya hivyo Novemba mwaka 2013 ikifuatiwa na Uifilipino. Kwa upande wangu nimepata faraja kubwa sana kwani tarehe 3 Januari mwka huu niliweka post  FB nikiitaka Serikali yetu Kuteketeza meno yaliyokamatwa na Kuiwekea msimamo mkali Serikali ya China, tarehe 6 Mwezi huu China imeteketeza tani 6 za meno ya tembo na Bidhaa zake. Hata kama hatua hiyo ya China haikutokana na Maoni yangu nimefarijika sana na hatua hiyo na narudi kuisihi serikali yetu iteketeze meno ya tembo yote yaliyokamatwa kama ilivyofanya Marekani, Ufilipino na China. Kwani Meno hayo yatawafikia kwa mlango mwiongine hao hao wanaohamasisha mauaji ya Tembo nchini kwetu. Aidha Serikali iiwekee msimamo mkali China juu ya tatizo hili kutokana na waqnanchi wake wengi kushiriki kuangamiza Tembo
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad