Katika
harakati za jicho la Kamera ilinasa 'Image' ya picha
ya Meli hii pichani isiyokuwa na jina wa kiashilio chochote cha
kuonyesha mahala inapotoka meli hii, jambo ambalo lisatengeneza maswali
mengi yasiyo na majibu kwa kila atakayepata fursa ya kuiona meli hii
ikiwa imetia Nanga eneo hili la nyuma ya Hoteli ya Kitalii ya Kunduch
Beach, jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau waliozungumza na Mtandao huu, walisema kuwa meli hiyo ina muda
mrefu sasa tangu walipoanza kuiona mahala hapo huku ikiwa haina
shughuli yeyote zinazoendelea kwenye Meli hiyo wala mhusika.
Aidha
imeelezwa kuwa Meli hiyo ni mali ya mfanyabiashara mmoja wa vyuma
chakavu, ambaye ameinunua kusikojulikana na kuitelekeza mahala hapo,
ambaye amekuwa akinunua meli kuukuu na kufanya shughuli ya kuzikatakata
katika eneo hilo pembezoni mwa hoteli ya Kunduchi Beach na kisha kuuza
vyuma chakavu.
Hakuna
baya katika hili kutokana na kwamba ni biashara ambayo inafanywa na
waliowengi kwa hivi sasa na wala si kosa la jinai, lakini kutokana na
kitendo cha kuachwa mahala hapa kwa muda mrefu tena pembeni mwa Hoteli
kubwa kama hii kinaacha maswali mengi tu yasiyokuwa na majibu.
1. Kwa nini mmiliki wa meli hii achague eneo la hoteli za kitalii kufanyia chinja chinja ya meli chakavu?
2. Je zoezi hilo halina madhara au haliathiri mazingira kwa namna moja ama nyingine?
3. Mamlaka husika wana habari ya zoezi hili?
4. Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ina habari juu ya zoezi la mfanyabiashara huyu katika eneo hili?
Hayo
ni baadhi ya maswali na mengine mengi yasiyokuwa na majibu ya haraka.
Jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugwimbana ili
kuzungumzia juu ya suala hili ziligonga ukuta baada ya kumtafuta kwa
njia ya simu na muda wote simu ikiwa bize ikiita bila majibu.
0 comments :
Post a Comment