.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

WALICHSEMA G NAKO NA JOH MAKINI KUHUSU SWALA LA LORD EYEZ KUSIMAMISHWA KAZI BAADA YA KUKAMATWA


Neno la G-Nako kama member wa Nako 2 Nako kuhusu Lord Eyez kusimamishwa kazi 'Weusi'


Kampuni ya Weusi kupitia msemaji wake, Nikki wa Pili leo imetangaza kumsimamisha kazi rapper Lord Eyez ambaye mbali na kuwa mwana hisa wa kampuni hiyo, ni member wa kundi la Nako 2 Nako toka Arusha.
Kama inavyofahamika kampuni ya Weusi ilikuwa inaunganisha rappers wa makundi mawili ya wanajeshi wa muziki mzuri toka Arusha, Nako 2 Nako Soldiers na River Camp Soldiers.
Kufuatia uamuzi wa Weusi, G-Nako ameeleza mtazamo wake pia kwa kuzingatia kuwa yule ni mwanafamilia mwenzake wa kundi hilo.
“Nafikiri alichokwambia Nikki ni kitu ambacho tumekubaliana watu wote na msimamo kama wa kampuni ndio huo.” Amesema G-Nako. “Haijalishi kama ni member, ni Nako 2 Nako ni nini lakini Lord Eyez ni mmoja wa wanahisa wa Weusi na kilichofanyika ni hicho na maamuzi ndio hayo, hilo swala liko ndani ya Kampuni.”
Baada ya Lord Eyez kusimamishwa kazi, hivi sasa Nako 2 Nako ina mwanahisa mmoja tu kwenye kampuni ya Weusi, huku wana River Camp wakiwa watatu.  Biashara inaendelea na sheria inafuata mkondo.
Hata hivyo, bado kuna mkanganyiko kati ya tafsiri ya tamko la Weusi kwa baadhi ya watu, ambapo wengi wamechukulia ‘kusimamishwa’ kama ‘kufukuzwa’. Hii imempelea Joh Makini kufafanua.
“Lord Eyez hajafukuzwa wala kutengwa kama wengi mnavyoitafsiri.” Joh Makini ameandika Instagram na kupost picha akiwa na Lord Eyez.
http://distilleryimage10.ak.instagram.com/9b36809ca3a611e38e671220bc4e24d2_7.jpg
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad