BAADA ya kibarua cha David Moyes kuota nyasi Manchester United, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amempa pole sana.
Moyes
amefanya kazi kwa miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka 6 na kocha
mchezaji Ryan Giggs ametangazwa kuwa kocha wa muda mpaka mwishoni mwa
msimu.
Louis van Gaal anapewa nafasi ya kuchukua nafasi hiyo, japokuwa anahusishwa kuhamia Tottenham.
Chaguo
la kwanza ni Jurgen Klopp ambaye leo hii imejitoa kuitaka kazi hiyo kwa
madai kuwa bado ana kibarua Borussia Dortmund mpaka mwaka 2018.
“Sipendi sana kuzungumzia. Nampa pole sana, ni kawaida’. Mourinho ameiambia ITV.
“Nampa pole David kama ninavyowapa pole makocha wengine wanaopoteza kazi”
Moyes
aliyevunja rekodi nyingi za Manchester United kwa muda mfupi aliokaa
Old Trafford, amekuwa kocha wa kwanza kutimuliwa tangu ilipotokea hivyo
kwa Ron Atkinson mwaka 1986.
0 comments :
Post a Comment