.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MRISHO NGASSA AMPELEKEA MPIRA WEMA SEPETU, NI ULE ALIOPEWA BAADA YA KUSHINDA HATRICK


WEMA
  “Diamond ni rafiki yangu, lakini mpira huu nitampelekea Wema kwa kuwa ni shemeji yangu na tunaheshimiana sana,” alisema Ngassa 
 Mrisho Ngassa wa Yanga, jana alifanikiwa kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika mechi dhidi ya JKT Ruvu, lakini ametoa kali kwa kusema kuwa mpira aliokabidhiwa kwa kufunga mabao hayo, anaupeleka kwa shemeji yake, Wema Sepetu. Akizungumza baada
ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa timu yake kupata ushindi wa mabao 5-1, Ngassa huku akionyesha kuwa na furaha, alisema kuwa mpira huo umeongeza hamasa kwa timu yake, lakini moja kwa moja atampelekea Wema ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond.

 “Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa na timu yetu, sisi tutapigana mpaka dakika ya mwisho ili kuhakikisha tunashinda mechi zote. Wakati mwingine tunashindwa kucheza vizuri mikoani kwa kuwa viwanja vinakuwa havina ubora mzuri.” 

 Yanga imepata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuamsha mbio za ubingwa dhidi ya Azam ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara, lakini kipa Juma Kaseja na mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi hawakuwepo kwenye kikosi kilichoanza wala kwenye benchi. -

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad