Wednesday, 9 April 2014

POLISI WAMTIMUA 'CHACHA' CHUO KIKUU

Ndugu Chacha Makene

CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
Chacha akionesha mahali lilipokuwa handaki lake.
Kana kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi katika handaki hilo kwa muda wa miaka mitano, alipotoka, alikuta makazi yake hayo yakiwa yamechomwa moto na vitu vyake vyote kuchukuliwa.
  kijana huyo alikiri kutokewa na mambo hayo na kulalamika kuwa kitendo alichofanyiwa, kimempotezea mwelekeo wa maisha yake kwani hana tena sehemu ya kwenda kwa kuwa hakujiandaa.
Alisema alipokamatwa alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kudhaniwa kuwa ni mgonjwa wa akili, lakini alipingana na madai hayo, licha ya kuwa aliishi kwa siku 36 hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa kuondoka.


 
Chacha akiketi kidandanda aliporipotiwa kwa mara ya kwanza
Chacha akifunga mlango wa handaki yalipokuwa makazi yake

No comments:

Post a Comment