Cristiano
Ronaldo anatarajia kurudia dimbali kuitumikia Real Madrid leo kwenye
mchezo wa awali wa nusu fainali ya Champions League dhidi ya Bayern
Munich katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Kocha
wa Madrid Carlo Ancelotti amesema atafanya maamuzi juu ya mchezaji huyo
mwenye miaka 29 ambaye alikosa michezo minne ya mwisho ya klabu hiyo
ukiwepo mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme ambapo Madrid waliishinda
Barcelona 2-1.
Naye Boss wa
Bayern Munich Pep Guardiola hajawahi kupoteza hata mchezo mmoja katika
michezo sita aliyocheza na Real Madrid katika dimba la Bernabeu.
Bayern Munich imeichapa Real Madrid mara nne katika michezo mitano ya nusu fainali ya European Cup ambapo timu hizo zimekutana.
Real
inajivunia rekodi yao ya kutwaa taji la Champions League mara tisa
lakini inalisaka taji hilo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 12.
0 comments :
Post a Comment