Monday, 30 June 2014

Rick Ross atupwa lupango masaa kadhaa North California

Rick Ross atupwa lupango masaa kadhaa North California
Kiongozi wa May Back Music ameripotiwa kuwa alikamatwa na kutupwa selo na polisi wa Greensboro, North California baada ya kumaliza show yake katika tamasha la SuperJam 2014.
Kwa mujibu wa TMZ, Rick Ross alikamatwa na polisi kwa kuwa hajaonekana katika mahakama za             North California kuhudhuria kesi yake inayohusu bangi/Marijuana iliyokuwa inamkabiri tangu mwaka jana.
Rapper huyo anadaiwa kuwa hakuonekana kabisa eneo hilo hadi mwaka huu, ambapo polisi wametumia nafasi hiyo kumkamata.
Hata hivyo, Rick Ross ambaye hivi sasa amepungua sana uzito anadaiwa kuwa mpole na kutii sheria hadi alipotupwa selo na kuachiwa masaa kadhaa baadae

No comments:

Post a Comment