.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

BIFU YA PEPE NA KEITA, YAINGIA KURASA MPYA..NUSURA WAZICHAPE UWANJANI..CHEKI FULL VIDEO HAPA

Mshike mshike wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma, uliingia katika mzimu wa mpambano wa mahasimu wakubwa nchini Hispania baada ya beki kutoka nchini Ureno Pepe kukwaruzana na kiungo kutoka nchini Mali, Seydou Keita.
Wawili hao walikwaruzana kabla ya mpambano huo wa kujiandaa na msimu haujachezwa katika mji Dallas, nchini Marekani ambapo Pepe alionekana akirushiwa chupa ya maji hali ambayo ilizua tafrani kabla ya kuamuliwa na wachezaji wenzao.

Pamoja na madhila yoye hayo Pepe alionekana ni mwenye kutabasamu na kuyapuuza yaliyotokea.
Hata hivyo kitendo hicho kilipelekea hasira kwa Keita na kujikuta akifanya maamuzi ya kutompa mkono Pepe wakati wachezaji wa AS Roma walipokuwa wakiwasalimu wachezaji wa Real Madrid kabla ya mchezo huo wa kirafiki kuanza.

Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji hao kukwaruzana, kwani kama itakumbukwa vyema wakati wa mchezo wa Spanish Supercopa wa mwaka 2011 kati ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid, Keita alilumbana na Pepe baada ya kuchukizwa na maneno ya kibaguzi ambayo alidai alitamkiwa na beki huyo kutoka nchini Ureno
Mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma ulichezwa usiku wa kuamkia jana, ambapo mabingwa wa barani Ulaya The Meringues walikubalia kulala bao moja kwa sifuri.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad