Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo aliyepo mkoani Tabora anakotokea Shilole, watu wanaomjua wamekuwa wakisikitishwa na matamshi yake kuwa ana mtoto mmoja.“Tumekuwa tukisoma na kumsikia akisema ana mtoto mmoja anayeitwa Rahma, lakini ukweli ni kwamba ana mwingine anayeitwa Joyce na wote kazaa na wanaume tofauti,” alisema ‘sosi’ huyo kutoka mkoani humo.Ili kupata mzani wa habari hiyo, The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shilole na baada ya kumpa mkanda mwanzo, mwisho, alikiri kuwa ana watoto wawili.“Ni kweli nina watoto wawili, Rahma na Joyce, wote wanasoma The Click International School,” alisema Shilole na alipoulizwa kwa nini amekuwa akisema ana mtoto badala ya wawili, alikosa jibu.
No comments:
Post a Comment