Monday, 15 September 2014

Mbowe Tena Chadema, Achaguliwa kwa Kishindo Kuongoza Chama Hicho

Freeman Mbowe amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chadema katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana.

Katika uchaguzi huo, Mbowe alipata kura 789 sawa na asilimia 97.3 na kumshinda mpinzani wake ambaye hakuwa na nguvu kubwa, Gambaranyera Mongateo aliyeambulia kura 20 sawa na asilimia 2.5

Hiki ni kipindi cha tatu kwa Mbowe kupewa ridhaa ya kuongoza chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Katika kinyang’anyiro hicho, wagombea walikuwa watano, wawili walienguliwa na mmoja, Kansa Mbarouk alijitoa.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa ukumbi ulilipuka kwa furaha ukihanikizwa na wimbo wa “Happy Birthday to you.” Jana pia ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa Mbowe akiwa amefikisha miaka 53.

No comments:

Post a Comment