Thursday, 6 November 2014

@Batuli asema "Ukimya wangu una sababu kubwa"

YobneshYusuf538BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, diva wa filamu za Bongo, Yobnesh  Yusuph  aka Batuli amefunguka kuwa ukimya wake una kishindo kwani kuna kitu kilimuweka bize hivyo watu wakae mkao wa kula atawasapraizi.
Batuli alisema hayo baada ya mashabiki kuuliza amepotelea wapi ambapo alisema kuwa aliamua kukaa kimya kidogo ili mashabiki wapate hamu ya kumuona kwani kitu alichowaandalia kiko njiani.“Ukimya wangu una sababu kubwa, nimeamua kufanya yangu ili mwisho wa siku nikiibuka nitoke na la kunitangaza,” alisema Batuli

No comments:

Post a Comment