UZINDUZI wa albamu ya Mwanamuziki Tarsis Masela, iitwayo 'Acha Hizo'unafanyika kesho
kwenye ukumbi wa Ten Lounge, zamani ulikuwa unaitwa Bunisiness Park, uliopo Victoria
Dar es Salaam.
Katika uzindu huo bendi ya Mashujaa, Akudo Impack na Jahazi Modern Taarab,
zitasindikiza usiku huo maalum wa Tarsis Masela.
Akizungumza Dar es Salaam jana Masela, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo
yamekamilika, huku akiwataka wapenzi wajitokeze kwa wingi kuangalia uzinduzi wake
\utakavyofana.
Masela ambaye ni Rais wa bendi ya Akudo Impact, anazindua albamu yake hiyo yenye
nyimbo saba, ambayo ni ya kwanza kuzindua na kuikamilisha.
Alisema kuwa kila mshabiki atakayekuja atapata burudani safi kutoka kwake na hata bendi
zinazomsindikiza.
Katika uzinduzi huo viingilio vitakuwa viwili ambavyo ni shilingi 30,000 kwa viti maalum na sh.10,000 kwa vya kawaida.
Katika albamu hiyo kuna nyimbo saba ambazo ni Tabia Mbaya ambayo amemshirikisha
Mzee Yusuf‘Mfalme’ Chaguo Langu, Nimevumilia Lady Jay Dee, nyingine ni Vidole
Vitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane.
Onesho hilo limedhaminiwa na RJ Company, Jambo Leo na Clouds Radio.
0 comments :
Post a Comment