Monday, 15 December 2014

KING MAJUTO AJIANDA KUMPIKU MR BEAN


Mkongwe wa Filamu za Vichekesho Tanzania, Amri Athumani 'King Majuto' amesema matarajio yake katika tasnia hiyo ni kuhakikisha anaongeza jitihada ili aweze kumpiku Mr Bean.

Mchekeshaji maarufu duniani Mr Bean
Majuto alisema hakuna mchekeshaji mwingine yeyote hapa duniani ambaye anaweza kushindana nae zaidi ya Mr Bean pekee. 

  "Katika tasnia hii watu wengi nawaona wa kawaida sana isipokuwa Mr Bean ambaye nipo katika harakati za kuhakikisha nampiku siwezi kukubali kushindwa," alisema Majuto.

 Pia, alisema umri unaenda, lakini nitahakikisha nastaafu tasnia hii wakati nipo katika nafasi nzuri.
Majuto alisema kwa upande wa Tanzania sanaa yake ni kubwa na ndiyo inayo muendesha maisha yake ya kila siku

"Mambo yangu sio mabaya kwa hapa nyumbani kwani Mungu anasaidia kutokana na kazi ninayoifanya kwani nina nyumba, gari na nimefanikiwa kujenga msikiti," alisema

No comments:

Post a Comment