.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

LE MUTUZ AFUNGUKA KUHUSU MISS TANZANIA KUFUNGIWA MIAKA MIWILI


Sitti Mtemvu Katikati akiwa na washindi wenzake katika shindano la mwaka 2014


Shindano la Miss Tanzania limesimamishwa kwa muda wa misimu miwili ili kutoa fursa kwa waandaaji wa shindano hilo kurekebisha baadhi ya kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa maraKaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza amesema kuwa serikali kupitia baraza hilo imefikia umamuzi huo kutokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau mbalimbali na wapenzi wa shindano hilo.
Amesema imefika wakati sasa waandaji warekebishe masuala kadha ili kuondoa malalamiko na manung'uniko miongoni mwa wadau ili kulipa heshima shindano hilo, pia liweze kuheshimika na kila mtu Mngereza ameongeza kuwa, serikali kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imelipa dhamana baraza hilo kisheria kushughulikia masuala yote yanahusu sanaa na Utamaduni hivyo baraza hilo lina mamlaka ya kuingilia kati endapo litajiridhisha kuwa kuna masuala hayaendi sawasawa.
Kuhusu masuala wanayotakiwa kuyarekebisha, Mngereza amesema kuna mambo mengi hayako sawa katika mchakato mzima kuanzia katika ngazi ya vitongoji, na baraza limekuwa likipata malalamiko karibu kila mwaka lakini kwa mwaka huu malalamiko yamekuwa mengi zaidi.
Mngereza amesema “Kama imefikia wakati hadi mshindi wa shindano mwenyewe analazimika kuvua taji lake kwa shinikizo, ina maana kuna tatizo, kwahiyo tumewapa muda ili wakaangalie upya mchakato mzima na wafanye marekebisho”
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, William Malecela (Le Mutuz) ambae pia ni mmoja wa waandaji wa shindano la Miss Ilala amekua na haya yakusema baada ya Miss Tanzania Kufungiwa miaka 2...

"Good Mornimg Instagram Nation I am coming live from Nduruma Farm Arusha resting U know....now Serikali kuifungia Miss Tanzania Miaka 2 what is that? Nani aliyefanya huo uamuzi? Hivi hili Taifa tuna nini vichwani? toka uamuzi utolewe naona watu wazima supposedly wenye akili timamu wanashangilia unashangilia nini you mazafantazz? Yaani kwa sababu hela.za Escrow zilipitia benk ya Kanisani Mkombozi basi na benki ifungiwe? Are U out of your gademu minds?.....So wasichana wetu wasishiriki mashindano yao wanayoyapenda kisa kuna Viongozi wa Miss Tanzania waliofanya makosa wewe unashangilia nini on that huoni kwamba ni uamuzi foolish absolutely nonsense.....ninasema hivi kwenye utafiti wao Basata ni wapi waligundua kwamba wenye makosa ni wasichana wetu wanaoshiriki? Nawaomba Basata wabadilishe uamuzi wao na wawafungie Viongozi tu au wawalazimishe kuwaachia wengine lakini kufungia mashindano yote miaka 2 kisa Lundenga hapana it is not right nasema huu uamuzi ni over reaction zaidi kuliko brainstorming kama ilivyotakiwa makosa ni ya Viongozi wa Miss Tanzania sio wasichana so fungia Viongozi sio Wasichana mimi nitalifikisha hili suala kwa Viongozi wakuu wa Taifa nikirudi tu Bongo it is not fair wasichana wetu kufungiwa kwa ujinga wa Viongozi wa Miss Tanzania it is gademu wrong! JAMANI ASUBUHI NJEMA SANA U KNOW! - le Mutuz"
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad