Charles Mihayo, (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi April, 20, 2014 aliwauwa watoto wake wawili wadogo wa kike nyumbani kwake huko Melbourne, Australia amehukumiwa kifungo cha maisha. Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi.
Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia. Kafungwa maisha na atatumikia miaka 31 kabla ya msamaha.
0 comments :
Post a Comment