Charity James
NYOTA wa muziki wa Hiphop nchini, Emmanuel Eribaliki ‘Ney wa Mitego’, amesema anatarajia kuachia video mbili tofauti za kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Akadumba’.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ney wa Mitego alisema kuwa sh. milioni 36 zimetumika kukamilisha video hizo ambazo anaamini zitakuwa kivutio kwa mashabiki wa kazi zake.
“Kiukweli kabisa imenigharimu fedha nyingi ambayo sikufikiria kama inaweza ikanigharimu kiasi hicho,” alisema Ney.
“Ni fedha nyingi zimenitoka lakini kikubwa nilikuwa natafuta kitu kizuri ambacho naamini kitawafurahisha mashabiki na wapenzi wa kazi zangu, maandalizi ya kazi hiyo yamekamilika muda wowote nitasambaza katika vituo mbalimbali vya redio,” alisema.
Alisema video moja ameifanya nchini Kenya na chini ya Mtayarishaji, Kelvin Bosco na nyingine alimsafirisha kuja Tanzania
Source: JamboLeo
0 comments :
Post a Comment