Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto)
akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty
linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es
Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Viti
Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige leo amezindua rasmi
rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina
la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika
barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua duka
hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke
Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina
alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha
ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote
nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa
umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa
wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa
nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.
Michuzi Media Group ikiongozwa Ahmad Michuzi mwanalibeneke wa Michuzijr Blog ( wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwanalibeneke wa Fullshwangwe Blog John Bukuku wakiwasili kwenye uzinduzi huo.
Aidha alitoa
rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji
ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia natoa
wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti
kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo
mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona fursa
za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa wito
kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo
nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani
fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya
ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hii”.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe
kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Mwana
Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George Meru (anayeshuhudia tukio
hilo).
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa
zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani
kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia
bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty
lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana
Diaspora Jestina George Meru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa
baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi
jana jijini Dar.
Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.
Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Wateja
wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo
vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of
Beauty.
Mkurugenzi wa ZuRii House of Beauty, Jestina George Meru akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
Mkurugenzi wa ZuRii House of Beauty, Jestina George Meru ( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.
Mkurugenzi wa ZuRii House of Beauty, Jestina George Meru akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya
kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha,
Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George Meru akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo jana.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo
Jestina George Meru kulia akizungumza na baadhi ya wanabloggers katika uzinduzi wa duka hilo .
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
0 comments :
Post a Comment