Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amekimbizwa hospitalini hapo Jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, baada ya kuwa mgonjwa, afisa ameiambia BBC.
Mr Kiir anasumbuliwa na matatizo ya kutoka damu puani, alisema afisa huyo. Maelezo zaidi ya hali yake hazipatikani.
Imebidi mkutano wa viongozi wa kanda kusogezwa mbele, waliitwa ili kujadili mgogoro wa Sudan Kusini, alisema afisa huyo.
Mr Kiir, 63, ameiongoza nchi tangu uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011.
Mr Kiir aliongoza mazungumzo mjini Addis Ababa Jumatano na kiongozi wa waasi, Riek Machar ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo vimeua maelfu ya watu tangu Desemba 2013.

No comments:
Post a Comment