Beki wa Bayern Munich, Medhi Benatia anafurahia sana kufanya kazi na kocha mkuu Pep Guardiola, akisema kwamba anajifunza vitu vipya kila siku kutoka kwa Kocha huyo wa Hispania
Beki huyo mwenye miaka 27 amejiunga na Bayern Munich akitokea Roma.
"Inavutia sana kufanya kazi na Guardiola." alisema beki huyo wakati alipokuwa anajibu maswali kutoka kwa mashabiki kupitia ukurasa wa Bayern Munich wa Twitter
"Kila siku unajifunza kitu kipya. Wengi wanaamini kuna kitu zaidi ya mchezaji wa Bayern anaweza kujifunza lakini siyo kesi kwa kocha kama yeye."Ni furaha kubwa."
Benatia pia akajibu maswali kuhusu mpinzani wake ngumu sana hadi sasa katika kazi yake ya Beki wa Kati alikiri kwamba mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic ndo amenisumbua zaidi.
"Ibrahimovic alikuwa mpinzani wangu mgumu. Yeye ndo mchezaji ambaye amenipa Matatizo sana.
"Yeye ni mchezaji mkubwa ambaye anaweza kujenga matatizo kwa timu yoyote." alisema Benatia.
Like our Facebook page CLICK HERE
Follow Twitter CLICK HERE
Follow Instagram CLICK HERE
0 comments :
Post a Comment