.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

JIBU LA LADY JAY DEE KWA MASHABIKI WAKE kuhusu, "Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio Na mpango wa kupatana nao."

Na hili ndo swali lapili alilojibu Msanii LadyJayDee, Ikumbukwe kwamba leo Lady Jay Dee anajibu maswali 10 alioulizwa na Mashabiki wake kupitia mitandao ya Kijamii, Kuliona swali lakwanza alilojibu CLICK HERE.
Endelea Kutembelea Blog Ya Vijana ili uweze kupata majibu ya msawali 10 alioulizwa Lady Jay Dee.


Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio
Na mpango wa kupatana nao :

JIBU :
"Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha. 
Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha 
Otherwise hakuna miujiza 
Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .
Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote 
Hakuna binadamu asie kosea 
Ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha. 
Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua .

Je! Hili jibu limejitosheleza? 
Naamini hata nyinyi mmewahi kutofautiana na watu wenu wa karibu. 
Kukubali kosa ndio mpango
"

Swali La 3 limejibiwa hivi 


Swali: Siasa 
Mchango katika jamii 
JIBU :
"Sio mpenzi na sitegemei kujihusisha na siasa, wala chama chochote. 
Kila binadamu ana mchango katika jamii kwa njia moja au nyingine. 
Direct au indirect. 
Ukitambua moja lolote nililowahi kulifanya likakupa furaha ndio mchango wangu, samahani kwa yaliokuudhi. 🙏🙏🙏🙏 Swali la 4 mpk la 10 ntamalizia kesho, yasipoisha hata kesho kutwa 
Najua kuna maswali mazito mnayosubiria majibu, yale ya kidaku zaidi. ...
Na mimi kwa kuwarusha roho nayaweka mwiiiishooo
Yatajibiwa tu, msitie shaka. ...
🙋🙌🙋🙋🙋🙌"



Afya na Urembo. 
Je! Nafanya diet na mazoezi? 
Nani ananipaka make up/nguo? 
JIBU : 
"Sifanyi diet nakula kuliko mwanaume 
Naweza kula kuku mzima for lunch tu 
Ila kuna baadhi ya vyakula sili 
Sili Pork 🙈🙈🙈Nguruwe @ivvycarter😂😂😂😂 Sili red meat, (Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Swala n.k) sili kabisa 👎👎👎👎👎👎👎👎👎👎👎 Lakini pia nakula
Mboga mboga na wanga za aina zote zinazolika, nakula tu.
Maisha yangu ni Kuku na Samaki zaidi
🐡🐡🐡🐡🐡🐟🐟🐟🐟🐟🐠🐠🐠🐠🐠🍗🍗🍗🍗🍗
Nakunywa alcohol kiasi, sio kupitiliza mpka nikaharibu, ni mpenzi wa Beer,Wine, Champagne. 
Siko kwenye pombe kali kali sana km ma whisky, na ma vodka, gin, brandy 
Hizo sio ishu zangu 
Sivuti sigara labda kiutani 
Navuta Sheesha for fun, once in a while km swags sio addict 
Je!mnasubiri niseme navuta ndwee?
I better ruuuuuuuun .

MAZOEZI : Sio addict, ila huwa nafanya inapobidi, kutokana na hali iliopo na watu nilionao kwa wakati huo 
Sit ups kwajili ya tumbo 
Kuruka kamba, karate nilipita kidogo na nategemea kujiunga na gym hivi karibuni km sitaskia uvivu.
Kwenye mazoezi naweza kujiita bendera fuata upepo. 
Lakini maisha yangu ni gym tosha, sababu nafanya kazi zote mwenyewe, kupika, kuosha vyombo, kupiga deki, ila sipendi kufua, sbb napenda kucha zangu. Huwa sifui labda chupi na uniform za Mokonyo ikibidi. 
MAKE UP :
Niliwahi kufanyiwa make up na Maya Janeska @maya_mia_y bdae Tonton Marcel 
Ila casualy huwa najipaka mwenyewe. 
Ninaposafiri ku shoot video, huwa nakutana na make up artists wa huko huko ninapoenda , wananihudumia. 
Pia Nimewahi kufanyiwa make up na Tuma @makeupby_tumakay 
NGUO :
Nanunua nguo yoyote inayonipendeza 
Zingine naletewa zawadi 
Zingine nashonewa na designers wa hapa hapa nyumbani (Tanzania )
Recently kwenye shows/ hafla kubwa kubwa nimekuwa nikivishwa na Tasleem wa South Africa 
NAFIKIRI HII NAYO IMEJITOSHELEZA 👊👊👊👊👊👊"



Unaweza jiunga nasi ili usipitwe na habari pindi pale ntakapokuwekea 

Like our  Facebook page CLICK HERE
Follow Twitter CLICK HERE
Follow Instagram CLICK HERE

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad