Amber Rose anataka kuweka sawa majibizano yanayoendelea na baadhi ya wanafamilia ya Kardashian.
Model huyo (31), alielezea drama hio baina yake na Khole Kardashian (30), ilioanza mwezi February katika mtandao wa twitter baada ya Rose kuongelea kuhusu mahusiano ya Kylie Jenner na rapper Tyga.
"Simchuki Khloe. Simchuki yeye," Rose alisema katika interview.
"Ndio, nisinge ingilia issue ya mdogo wake na mahusiano yake. ila mimi nimekuwa dancer katika umri mdogo na kujihusisha na wanaume wakubwa, ilinipa nguvu na akili ya kuzungumzia issue kama hio," alieleza Amber Rose.
Ila Hakuishia Hapo.
"Naweza kuelewa kwanini imefika kivingine kwake. Naelewa. ila ilikuwa anipigie tu simu nakunielewa, hakutakiwa kuTweet mara 11 na kuni dhalilisha wakati sababu peke inayowafanya hawa wasichana kuwa na career nzuri ni kutokana na dada yao mkubwa kujirekodi video." Rose aliendelea kumchimba Kim Kardashian West ambae ni mke wa Kanye West ( X wa Amber Rose)
"Tuwe wakweli....sijawahi kuchukia swala hilo," aliongezea.
Ila mwana hip hop huyu bado aneleza kwamba yupo tayari kumaliza tofauti na mastar hao. Alipoulizwa kama yupo tayari kupatana na Kardashian, Rose alijibu, " Kabisa."
Oh, Pia alisema 100% hana tatizo na Kim
0 comments :
Post a Comment