Sunday, 22 March 2015

Breaking News: Mh: Zitto Kabwe ajiunga na chama hicho cha Siasa Tanzania


Mwanzoni mwa wiki Mh: Zitto Kabwe alivuliwa uwanachama wa Chadema na kumfanya kutokuwa na nguvu ya kubaki bungeni. 

Spika wa Bunge la Tanzania alimpa nafasi Zitto Kabwe kuwaaga wana siasa wenzake ndani ya Bunge kabla ya kuondoka bungeni

Asubuhi ya leo Taarifa kutoka ukurasa wa  Clouds fm uliandika taarifa ya Zitto kujiunga na chama cha Siasa cha ACT.

"Zitto Kabwe ajiunga rasmi na chama cha ACT-Tanzania asubuhi hii akabidhiwa kadi namba 007194." Iliandika Ukurasa wa Clouds fm Radio

No comments:

Post a Comment