.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Wivu wa Mapenzi. Nyumba, Magari yateketezwa na Moto jijini Arusha

Mtu mmoja ameuawa na nyumba mbili na magari matatu kuteketezwa kwa moto katika vurugu zilizotokea eneo la OLASITI jijini Arusha ambazo chanzo chake kinadaiwa kuwa wivu wa mapenzi.

Vurugu hizo zinadaiwa kusabiswa na makundi ya vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa jamii ya kimaasai maarufu kama “MORANI” katika eneo la OLASITI jijini arusha, wanaodaiwa kwa kukasirishwa kwa kitendo cha kuuwawa kwa mkazi wa eneo hilo kwa sababu ya mahusiano ya kimapenzi.


Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha kamishna msaidizi Edward Balele amesema baadhi ya watu wamekamatwa wanaotuhumiwa ka mauaji ya kijana melita wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na jitihada za uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendele.


Source: ITV

Stori hii imeenea mitandaoni siku ya Jana, wengi wakielezea Chanzo kuwa ni Baba mwenye nyumba hizo kusababisha kifo cha Kijana Huyo...

"Father house amerudi nyumbani akakuta house girl anakula uroda na kijana wakimasai wa hapo hapo mtaani. Si akamwitia mwizi akiwa na rafiki zake wakamshushia kipigo cha mbwa mwizi walipo kuja wasamaria waka mtetea dogo kuwa mbona hana record ya wizi ndipo wakaelezwa ilivyokuwa baada ya kupelekwa hospital masai kafa. wale jamaa zake walipo juwa si ndio wakapuriza tarumbeta lao la kukusanyika walipo jikusanya wakaanza kwenda kutia hasara kwa wale waliouwa." iliandika moja ya Ukurasa 


Tuachie Comment Yako
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad