Beki wa kulia wa klabu ya Barcelona, Daniel Alves kubaki na klabu yake hio japo mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu, kwa mujubi wa mwanachama wa tume ya kiufundi ya klabu.
Mkataba wa mbrazil huyo ndani ya Camp Nou unakaribia kuisha na maongezi kuhusu mkataba mpya hayajafanikiwa mpaka sasa.
Wakala wa Dani Alves, Dinorah Santana, alisema mwezi April kwamba Offer ya Barcelona haikuridhisha na majadiliano yalivunjika, huku Alves akitalajiwa kuondoka baada ya msimu kuisha.
Offer ambayo Alves alikataa ilikuwa apewe mkataba wa mwaka mmoja mpaka miwili kisha kama hatocheza asilima 60 ya mechi za barca msimu ujao basi hato hesabiwa kama mchezaji wa barcelona msimu unaofata. Alves alikataa offer io yamwisho kutoka barca kwani wakala wake ambae ni mke wake wazamani alisema kuna klabu 3 zinazoshiriki UEFA tayari zimemfata Dani ila alikuwa anasubiri offer yamwisho kutoka Barcelona.
Hata ivyo, Charles Rexach, aliiambia Esports Cope kwamba ana matumaini makubaliano yatafikiwa.
"Mimi ni mmoja wa watu ambao bado namuona (alves) msimu ujao. Nashawishika Dani Alves atabaki Barcelona," alisema Rexach
Beki huyo wa kulia alijiunga na Barcelona akitokea Sevilla mwaka 2008 na amecheza zaidi ya mechi 300 kwenye mashindano yote ya klabu hio.
Alves alikuwa miongoni mwa kikosi kilicho shinda La Liga, Copa Del Rey, Champions League, Supercopa de Espana, European Supercup na Club World Cup mwaka 2009.
Blog ya Vijana ipo kukuletea habari zote unaweza tufollow Instagram na Twitter kisha Like page yetu ya Facebook ili usipitwe na habari zetu, kwa chcochote tuachie comment yako au tutumie email....
0 comments :
Post a Comment