Monday, 29 June 2015

Sakata La De Gea bado


MANCHESTER United imeridhia golikipa wake David de Gea kuondoka ndani ya kikosi hicho lakini ziwekwe mezani kiasi cha pauni milioni 35 (Sh. 125,801,849,103.98), huku Real Madrid ikikataa kulipa kiasi hicho.

 

Real Madrid ndio wanaomtaka mno golikipa huyo na Manchester United inadaiwa wamekomaa katika kiasi hicho na wapo tayari kumpoteza bure msimu ujao.

 

Kama atafanikiwa kuondoka kwa kitita hicho, atakuwa ameandika rekodi ya dunia na kuivunja ile ya Gianluigi Buffon aliyoweka mwaka 2001 wakati akitoka Parma na kutua Roma alipochukuliwa kwa pauni milioni 32.6.


 


Old Trafford wanaamini hicho ndicho kiasi sahihi kwa Real Madrid kutoa kama wanamtaka mlinda mlango huyo na iwapo wakiona ni kikubwa wasubiri mwakani wamchukue bure.

 

De Gea alijiunga Manchester United mwaka 2011 kwa kitita cha pauni milioni 17.8 na sasa anataka mno kurejea nyumbani Hispania.

 

Lakini Real Madrid jana walisema hawana uwezo wa kulipa kiwango hicho kinachotakiwa na Manchester United.

No comments:

Post a Comment