Sunday, 28 June 2015

Vanesa Mdee awapa neno wanaotumia Dawa za Kulevya



STAA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Vanesa Mdee, ‘Vee Money,’ amewashauri wasanii wenye tabia ya kutumia dawa za kulevya wanapofanya maonesho mbalimbali kutofanya hivyo.

Akizungumza na gazeti la Staa Spoti, Vee amesema msanii ni kioo cha jamii, hivyo hapaswi kufanya mambo yasiyofaa.



“Kwa kweli sijui kama kuna wasanii wanaotumia dawa za kulevya wakiwa kwenye maonesho, sijawahi kuwaona, kama wapo, wanatakiwa kuachana na tabia hiyo, maana kuna watoto wadogo ambao wanakua, wanataka kufanya kama anavyofanya msanii fulani, sasa hiyo ni mbaya,” anasema.

Vee Money amewataka wasanii wenzake kufanya vitu ambavyo ni mfano wa kuigwa kwa jamii inayowazunguka.



Anasema wasanii wanaangaliwa kama kioo cha jamii, hivyo wanatakiwa kuwa viongozi muhimu katika jamii kupitia kazi wanazozifanya wawapo mitaani, majukwaani, na hata na familia zao.
 
 
 
Link (Click Here) to Vote
 


No comments:

Post a Comment