.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Zari: Watanzania naomba msinifatilie



Mpenzi wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' aitwae Zarinah Hassan 'Zari' amewaomba watanzania kuacha kumfatilia maisha yake.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuandamwa na mashabiki kutokana na uvaaji wake na kuwaomba wamuache kama alivyo kwani amechoka na maneno yao.



Kupitia ukurasa wake  wa mtandao wa kijamii, ameandika "Maisha yangu yanakuhusu nini wewe, na yako hayanihusu ata kidogo ooh viatu virefu, mara nguo imebana, pili pili hujakula wewe inakuwashia nini? Mvae madera zenu mfunge mkanda mpite kimya???

Alisema ayafanyayo ni maisha yake binafsi na Mungu pekee ndiye wa kumuhukumu na sio binadamu.
"Watu wangapi wanavaa hijabu lakini bado wanamkufuru Mungu, ni watu wangapi wanakuwa wasafi kwa siku 30 lakini ndani ya miezi 11 wanakuwa waovu," alisema na kuongeza



"Nawashangaa watu wanaovamia ukurasa wangu na kuanza kuhukumu mavazi yangu, siwezi kumzuia mtu kukosa lakini sitaki kuvamiwa katika ukurasa wangu na kuanza kupolomoshewa matusi." 
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad