Monday, 6 July 2015

Steve Nyerere akomalia wanaombeza


Nyota wa filamu nchini, Steve 'Nyerere' Mengele, amesema kuwa wanaobeza uamuzi wake wa kuwaniaubunge waendelee, lakini yeye ameutaka na amejipanga kuhakikisha anaupata.

Hivi karibuni msanii huyo alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akidai kuwa ni mwanachama wa siku nyingi wa chama hich tawala.


"Napenda kusema kwamba sijakurupuka na wala sijatangaza nia yangu ili tu kupata sifa eti kwa sababu labda nimeona mtu fulani amegombea na mimi basi tu nigombee, hapana. Nimeona katika wilaya yangu ya kinondoni kuna matatizo kadhaa na naweza kuwa suluhisho," alisema

No comments:

Post a Comment