Fikiria ni jinsi gani wageni wanapata shida kutambua ni yupi anaongea nae pindi akiingia kwenye nyumba ya familia yenye makazi yake Moscow, Idaho, ambapo ndugu mapacha Phil na Doug Malm wanaishi na wake zao Jena na Jill ambao pia ni mapacha.
Wapenzi hao wote wanaishi chini ya paa moja, mtoto mmoja kila wapenzi - na watoto wao wanafanana.
Wanaume (58), wanawake (48) walifunga ndo mwaka 1993 katika sherehe ya mapacha - mkusanyiko mkubwa wa mapacha duniani, huuzuliwa na mapacha zaidi ya 3000 kila mwaka.
Mapacha hao walirudi tena katika sherehe hizo zinazofanyika Twinsburg, Ohio kusherekea maadhimisho ya miaka 22 ya mapenzi yao.
Phil na Doug, ambao wameishi pamoja maisha yao yote, waliwakuta Jena na Jill Lassen katika sherehe hizo mwaka 1991.
Katika sherehe za mwaka ujao (1992) mapacha wakiume walipanda kwenye stage, na kuchukua kipaza sauti na kupendekeza ndoa kwa wachumba wao mapacha.
Mwaka 1993 kabla wapenzi hao hawajafunga ndoa, Phil alisema;
'Watu hawaelewi kwanini tunataka kuishi pamoja, Ni bond ya mapacha tulionayo amabayo hatuna tatizo nayo.'
Doug akaongezea: ' Watu huwa wanatuuliza kama tupo huru, na mimi nawaambia tupo huru tena sana.'
Phil na Jena wana mtoto wakiume, Tim, huku Doug na Jill wana mtoto wakike, Rylie. Japo watoto hao ni mabinamu kinamna, wao ni ndugu wa damu moja.
Familia hii ya mapacha sio mfano peke wa mapacha wakiume kuoa mapacha wakike.
Melanie na Rachel walifunga ndoa na wahandisi wa petroli Nathan na Scoot - pia ni mapacha, (Wamehudhuria sherehe za mapacha kwa miaka minne mfululiz.
0 comments :
Post a Comment