Msanii maarufu anayetisha kwa miondoko ya R&B kutoka nchini Marekani, Ne-Yo ameacha gumzo kwa wapenzi wa muziki wanaofatilia onyesho la Coke Studio kutokana na manjonjo anayofanya akiwa jukwani katika kolabo aliyofanya pamoja na wasanii wengine wa Africa.
Mwanamuziki huyo ambaye ni msanii mwalikwa kwenye msimuhuu wa coke Studio, anatamba na vibao vyake na vibao vyake mbalimbali vya 'Let Me Love You', 'Beautiful Monster', 'Coming With You' na 'She Knows ft Juicy J'.
Baadhi ya vijana waliozungumzia kolabo hiyo, walisema kuwa Coke Studio imenoga na kuvutia wengi kutokana na kumshirikisha mkali huyo wa sauti ( Ne-Yo).
"Kollabo la Ne-Yo na wanamuziki wengine wakali kutoka Afrika ni Ubunifu wa aina wake katika onyesho la Coke Studio unatoa fursa ya kuwawezesha wanamuziki wachanga kujiamini katika kufanya kazi za kimataifa," alisema Julius Joseph, Mwanfunzi wa chuo cha Biashara Dar es salaam anayefuatilia onyesho hilo.
0 comments :
Post a Comment