Tinga tinga takribani tatu zipo katika Bonde la Mto msimbazi katika eneo la Mkwajuni jijini Dar es salaam zikiendelea na kazi ya kubomoa nyumba zilizojengwa katika eneo hilo.
Bonde la Mto msimbazi ni moja ya eneo linalodaiwa kuwa hatarishi kufuatia kujaa maji ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vya watu hasa katika msimu wa mvua.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi mwishoni mwa mwaka jana alitoa siku 14 kwa wakazi wote wa mabondeni kuondoka kabla serikali haijachukua hatua kali ikiwemo kubomoa nyumba hizo.
Aidha, siku ya 14 leo tarehe 5 ndiyo mwisho ambayo serikali imeanza kwa kasi kubomoa nyumba zilizojengwa katika maeneo hatarishi.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi katika Bonge la Mkwajuni wameiomba serikali kuwapatia muda katika maeneo hayo hatarishi ili wajipange kutimiza maagizo hayo ya serikali yanayowataka kuhama haraka iwezekanavyo.
0 comments :
Post a Comment